Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kesho uwanja wa Azam Complex kuipa sapoti timu yao katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc
Azam Fc na Yanga zitakutana katika mchezo wa kwanza wa kukata na shoka msimu huu
Timu hizo ziko juu ya msimamo wa ligi zote zikiwa zimejikusanyia alama 25 Azam Fc wakiongoza kwa tofauti ya mabao
Bumbuli amesema Wanayanga hawapaswi kuwa na hofu kuelekea mchezo huo kwani ana uhakika alama zote tatu zitakuwa zao
"Msimu huu tumedhamiria kuweka rekodi, Azam Fc hawana timu ya kutufunga, hivyo mashabiki tujitokeze kwa wingi tujaze 'kauwanja kao' na baadae tuondoke na alama zetu tatu," alitamba Bumbuli
Mshindi wa mchezo huu atajipambanua kileleni mwa msimamo wa lig na pia ndiye atakeyekuwa mbabe mpya wa dabi zilizokutanisha timu hizo
Katika mechi walizokutana kabla, Azam Fc wameshinda nane na Yanga wakishinda nane pia. Timu hizo zimetoka sare mechi nane