Wananchi wamempa Injinia Hersi Said kazi moja tu, kuhakikisha dirisha dogo anamleta Heritier Makambo kuongeza nguvu kwenye kikosi cha ubingwa msimu huu
Bado safu ya ushambuliaji ya Yanga imeonekana kuwa na changamoto, matumizi ya nafasi sio kwa kiwango kinachoridhisha
Tangu atue kocha Cedric Kaze, Yanga imerejesha utamaduni wa kushambulia kupitia pembeni
Jana peke yake kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc, beki Kibwana Shomari alipiga krosi nne au zaidi
Enzi za kocha Mwini Zahera Yanga ilikuwa haitengenezi nafasi nyingi lakini hizo hizo chache Makambo alizitendea haki
Makambo alimfanya Ibrahim Ajibu kuwa staa Yanga, kwani krosi zake nyingi alikuwa akiziweka kambani
Ni wazi huyu mwamba akirejeshwa ataongeza ufanisi katika umaliziaji hasa mipira ya krosi
Ukiwa na Makambo, Michael Sarpong na Yacouba Sogne, hapa mabao lazima yatapatikana