Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said, amedokeza mfumo wa uendeshaji ambao Yanga huenda ikaenda nao
Hersi yuko Hispania akitarajiwa kukabidhiwa rasimu yenye mapendekezo yaliyotolewa na La Liga juu ya mfumo ambao Yanga inapaswa kujiendesha
Hersi amedokeza kuwa kuna aina tatu za mifumo ya uendeshaji. (1) Klabu inayoendeshwa na Wawekezaji kwa asilimia 100 (2) Klabu inayoendeshwa na Wanachama kwa asilimia 100 na (3) klabu inayoendeshwa na Wanachama (51%) na Wawekezaji (49%)
Amedokeza kuwa mfumo wa tatu ndio unaonekana kuwa na faida zaidi kulinganisha na mifumo mingine
Aidha, mfumo huo unakwenda sambamba na matakwa ya Serikali ya Tanzania kuhusiana na masuala ya uwekezaji kwenye vilabu vya soka nchini
Hisa asilimia 51% zitakuwa mikononi mwa Wanachama wakati asilimia 49% zitakuwa mikononi mwa wawekezaji
Wawekezaji watakuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya kifedha pamoja na kiutawala
Hata hivyo Wanachama wa Yanga ndio watakaoukuwa na sauti ya mwisho kuhusu utaratibu ambao wanataka klabu yao iendeshwe
Utakuwepo muda wa Wanachama kuelimishwa faida na hasara za kila mfumo kabla ya kufanya maamuzi kwenye mkutano mkuu ambao utaitishwa kwa ajili ya kupitisha ajenda hiyo