Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amewaalika mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mtanange utapigwa kuanzia saa 10 jioni
Aidha, Kaze amewapongeza mashabiki kwa kuiunga mkono timu yao katika mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc akiwakabidhi ushindi uliopatikana kwenye mchezo huo
"Ushindi dhidi ya Azam Fc ni wenu Wananchi popote mlipo. Tunaendelea kupambana ili kurudisha heshima kwenu na kwa sisi wote," alisema Kaze
"Tunaomba mujitokeze kwa wingi kutuunga mkono kwenye mchezo unaofuata dhidi ya JKT Tanzania. Mapambano anaendelea"
"Furaha yenu ndio heshima yetu"
ADVERTISE HERE