Ni mwendo wa burudani tu kwa mashabiki wa Yanga ambao baadae leo kikosi chao kitakuwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom, raundi ya 13
Ushindi katika mchezo dhidi ya Azam Fc umeongezea morali wachezaji ambao bila shaka leo hawatakuwa na mpango mwingine zaidi ya kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu pale kwa mkapa hivyo kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi
Kocha Cedric Kaze huenda akarejesha kikosi chake kilichoanza mchezo dhidi ya Azam Fc. Yacouba Sogne na Ditram Nchimbi waliongoza safu ya ushambuliaji katika mchezo uliopita
Safu ya ulinzi huenda Said Juma Makapu akaanza sambamba na nahodha Msaidizi Bakari Nondo, kutokana na Mghana Lamine Moro kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano
Mabadiliko mengine yanayotarajiwa ni safu ya ulinzi upande wa kulia, Kibwana Shomari akikosekana baada ya kuumia bega mchezo dhidi ya Azam Fc
Paulo Godfrey 'Boxer' au kiraka Deus Kaseke mfungaji wa bao pekee la Yanga kwenye mchezo dhidi ya Azam, huenda wakapewa majukumu hayo
Huu ni mchezo ambao Wananchi wana shauku kubwa kuona timu yao inaondoka na alama zote tatu
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi Alasiri ili kuwapa mashabiki fursa ya kushuhudia mchezo wa kombe la Shirikisho Ssaa moja jioni Namungo Fc watapepetana na Al Rabita ya Sudani Kusini