Wanayanga leo watampokea kiungo wao mshambuliaji Saido Ntibazonkiza raia wa Burundi
Ntibazonkiza atatua nchini majira ya saa 3:40 usiku na atapokewa na viongozi waandamizi wa Yanga wakiambatana na mashabiki wao
Ujio wa Ntibazonkiza ni faraja kwa Wanayanga kwani wanafahamu anakwenda kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji
Katika mechi tano zilizopita, akiwa na timu ya Taifa ya Burundi, Ntibazonkiza aliweka kambani mabao manne
Ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa kwani amecheza soka la ushinda barani Ulaya kwa zaidi ya miaka 10
Hapa tunamzungumzia mchezaji ambaye amecheza ligi kuu za Ubelgini, Uturuki na Ufaransa
Ujio wake Yanga ulifanikishwa mwezi Oktoba na GSM wakimnasa mda mfupi baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya Burundi ambao ulimalizika kwa Burundi kushinda bao 1-0. Bao ambalo liliwekwa kambani na Ntibazonkiza
Huu ni mtambo wa kufyatua na kutengeneza mabao...!