Kocha wa zamani wa Yanga George Lwandamina anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Azam Fc
Lwandamina ametua usiku wa kuamkia leo kujiunga na Wana rambaramba hao
Baada ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu, Azam ilimtimua aliyekuwa kocha mkuu Aristica Cioaba
Wakati akiwa kocha wa Yanga, Lwandamina alishinda ubingwa wa ligi kuu mwaka 2017
Pia aliiwezesha Yanga kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho
Lwandamina ni miongoni mwa makocha waliokuwa wameomba kuinoa Yanga wakati wa mchakato wa kumsaka mrithi wa Zlatko Krmpotic
Anarejea nchini kwa mara ya pili lakini sasa akiwa timu tofauti na Yanga
ADVERTISE HERE