Ujumbe wa Dominick Albinus kwa Wanayanga wote. Alibinus ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga na Mwenyekiti wa kamati ya ufundi
WANANCHI SHITUKENI
Mashabiki wa soka Tanzania hasa wa Yanga wamesahau kuwa wachambuzi hawa ndio waliwaambia Yanga mwaka hii hawawezi kushindania ubingwa
Ndio hawa hawa walisema huu ni msimu wa kujenga timu. Ndio hawa hawa walisema Yanga isijilinganishe na Simba kuwa imeachwa mbali sana
Tuliambiwa huwezi kusajili timu nzima ukategemea ubingwa. Mwingine akasema ili Yanga abebe ubingwa akasajili wachezaji waliopo benchi la Simba (Dharau sana)
Leo wameumbuka, sasa wanasema Yanga inashinda goli mojamoja, wamesahau walisema Yanga haina ubavu wa kuwania ubingwa!
Yanga imecheza mechi ngumu mfululizo na kutumia nguvu kubwa, lakini bado tunawalaumu wachezaji? Kuanzia mchezo wa Simba, Namungo, Azam Fc, JKT Tanzania tena mechi tatu katika kipindi cha siku nane bado hatuelewi?
Ni kweli watu hatuheshimu mpira kwa kuurahisisha sana lakini wachezaji wako tayari kupata muunganiko huku wakitumia nguvu kubwa kuhakikisha wanapata matokeo yatakayowawezesha kutwaa ubingwa
Tumerahisisha sana mpira kiukweli mpaka tunauvunjia heshima...!