Habari iliyotamba kwenye mitandao ya kijamii jioni ya jana ni kufungiwa miezi sita kwa aliyekuwa mchezaji wa Simba Shiza Kichuya ambaye sasa anaitumikia klabu ya Namungo Fc
Kichuya amefungiwa na Shirikisho la soka Duniani (FIFA) baada ya kuachana na klabu ya Pharco Fc ya Misri bila ya kufuata taratibu
Aidha klabu ya Simba imepigwa faini ya zaidi ya Tsh Milioni 300 baada ya kupatikana na hatia ya kumsajili mchezaji huyo bila ya kufuata taratibu
Taarifa ya FIFA imeeleza kuwa Simba ilimsajili Kichuya bila ya kupata baraka za Pharco Fc, yaani hakuwa na kitu kinachoitwa kwa kimombo 'release letter'
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaweza kuingia kwenye kashfa kwa kumruhusu mchezaji huyo kuitumukia Simba pasipo kuwa na viambatanisho muhimu kuthibitisha usajili wake
Hili ni kesi nyingine ambayo inakwenda kuwaachia maswali wadau wa soka nchini, Kichuya aliwezaje kuruhusiwa kuitumikia Simba wakati akiwa ni mchezaji halali wa Pharco Fc?
Lakini wakati haya yakitokea, klabu ya Yanga nayo ilipelekea mashitaka Mahakama ya usuluhisi wa michezo (CAS) wakipinga Mghana Bernard Morrison kusajiliwa na Simba wakati akiwa na mkataba halali na Yanga. TFF iliidhinisha usajili wa Morrison Simba
Yanga pia ilifungua mashitaka mengine kuhoji uhalali wa mkataba kati ya Simba na Morrison ambao unaelezwa haukuwa na saini kutoka kwa kiongozi yeyote upande wa klabu ya Simba
Ni mapungufu yanayofanana na hayo ndiyo yaliyotumika kuubatilisha mkataba wa miaka miwili ambao Morrison alisaini Yanga. Ilielezwa katika mkataba huo baadhi ya nakala zilikosekana huku saini ya Mwenyekiti nayo ikikosekana
Jambo jema ni kuwa kule FIFA na CAS hakuna ubabaishaji, kilichowatokea Simba kwa Kichuya kinaweza kuwatokea tena kwa Morrison
Mzaha huu kwenye usajili ipo siku utazigharimu hizi timu ikiwemo kuzuiwa kusajili, kunyan'ganywa pointi na pengine hata kushushwa daraja