FT : Mwadui Fc 0-5 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Dec 2020
FT : Mwadui Fc 0-5 Yanga

Wananchi wametakata uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga wakiibuka na ushindi wa kishindo kwa kuwafunga Mwadui Fc mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Yanga sasa imeanza kuwapa furaha mashabiki, kandanda safi na mabao yakianza kufurika

Kikosi cha kocha Cedric Kaze kilitawala mchezo huo kwa muda mwingi, wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Deus Kaseke na Yacouba Sogne

Kaseke na Sogne wameendelea kuinogesha Yanga kwani ushirikiano wao dimbani kwa mara nyingine umeinufaisha Yanga

Kaseke alifunga bao lake la tatu kwa pasi ya Sogne ambaye hiyo ilikuwa assist yake ya tatu kwa Kaseke

Aidha Sogne leo alikuwa mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Mwadui, ndiye aliyeongeza bao la tatu mwanzoni mwa kipindi cha pili, likiwa ni bao lake la pili siku ya leo

Mabao mengine ya Yanga yalifungwa na Tuisila Kisinda na nahodha Lamine Moro aliyemalizia krosi  murua ya Farid Mussa

Ulikuwa ni mchezo ambao Wananchi walicheza kwa mamlaka, hakika kikosi hiki kukifunga utahitaji kufanya kazi ya ziada

Ushindi huo unawaimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi wakifikisha alama 37

Mchezo unaofuata ni Jumamosi ijayo dhidi ya Dodoma Jiji, utapigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
37m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’