Wakati dirisha dogo la usajili likitarajiwa kuwa wazi kuanzia saa sita kamili usiku wa leo, Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema watatumia dirisha hili kufanya maboresho ya kikosi
Akizungumza na mkoani Singida jana, Hersi alisema tayari wamekamilisha usajili wa nyota Saido Ntibazonkiza ambaye anaweza kuanza kutumika kwenye ligi kuanzia mchezo ujao dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa mkoani Arusha Disemba 19
Aidha, Hersi amedokeza kuwa wapo wachezaji ambao wanawafuatilia na kila kitu kitakapokuwa sawa wataweka hadharani majina yao
"Tunafahamu dirisha dogo la usajili linafunguliwa kesho (leo), sisi tayari tumesajili mchezaji mmoja ambaye ni Saido Ntibazonkiza. Kama mambo yote yatakuwa sawa, tunatarajia Jumamosi atakuwepo uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji kule mkoani Arusha"
"Wapo wachezaji tutawatoa kwa mkopo ili wakapate changamoto zaidi, lakini pia wapo wachezaji ambao tunawafuatilia, mambo yakikamilika taarifa rasmi itatolewa, " alisema Hersi
Inaelezwa Yanga inaweza kuongeza wachezaji wengine wawili au watatu katika kipindi hiki cha dirisha dogo