Winga hatari wa Yanga Tuisila Kisinda ameeleza kufurahishwa na ari ya mashabiki wa timu hiyo ambao wakati wote hamasa yao inawafanya wapambane
Kisinda aliyetua Yanga akitokea klabu ya AS Vita ya DR Congo, amesema sasa ameelewa kwa nini mashabiki walijitokeza kwa wingi uwanja wa Ndege kuwapokea pale walipowasili
Amesema Yanga ni timu ambayo muda wote ina uhitaji wa matokeo. Ukaribu wao na mashabiki unawaongezea ari ya kuipigania timu
"sasa naelewa kwanini tulipokelewa vile uwanja wa ndege. Yanga ni timu ambayo muda wote ina uhitaji wa matokeo mazur"
"Mashabiki kila kona wanatutazama kwa jicho la ushindi na si vinginevyo. Hii inatufanya sisi wachezaji, benchi la ufundi na uongozi kwa ujumla kujiona tuna deni la kuwapa ubingwa mashabiki wetu," amesema Kisinda
Winga huyo mwenye kasi zaidi kwenye ligi kuu ya Vodacom, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Dodoma Jiji Jumamosi
Alipata majeraha madogo katika mchezo uliopita dhidi ya Mwadui Fc, alipewa mapumziko ya siku chache ili kupona majeraha hayo