FT : Yanga 3-1 Dodoma Jiji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Dec 2020
FT : Yanga 3-1 Dodoma Jiji

Wananchi wametakata uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakiwafumua Dodoma Jiji mabao 3-1 katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa jioni ya leo

Yanga ilikuwa nyuma baada ya dakika tatu Dodoma Jiji wakifunga bao la kuongoza kupitia kwa Seif Karihe aliyewahi mpira uliotemwa na mlinda lango Metacha Mnata katika shambulizi ambalo halikuonekana kuwa na hatari

Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha wananchi kuanza msako wa bao la kusawazisha

Iliwachukua dakika 27 tu Yanga kusawazisha bao hilo kupitia kwa nahodha Lamine Moro aliyemalizia vyema mpira wa adhabu uliopigwa na Deus Kaseke

Mpaka mapumziko ubao ulisomeka 1-1 pamoja na Yanga kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa

Saido Ntibazonkiza, hili jina itabidi watangazaji na wachambuzi wa soka nchini walizoee kwani dakika zake 45 alizopewa na Cedric Kaze kwenye kipindi cha pili, zilitosha kuipa Yanga alama tatu muhimu

Alifunga bao la pili kupitia mpira wa adhabu na kutengeneza bao la tatu kupitia mpira wa adhabu ambao uliwekwa kambani na Bakari Nondo Mwamnyeto

Ulikuwa ni mchezo uliogubikwa na matukio mengi ya kibabe kutoka kwa wachezaji wa Dodoma Jiji, itoshe kusema mwamuzi hakuumudu

Muhimu ni matokeo ya ushindi kwa Yanga ambayo imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha alama 40

Kwa hakika huu moto hautazimika mpaka sherehe za ubingwa mwezi Mei....!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’