Wananchi wana jambo lao Mbeya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Dec 2020
Wananchi wana jambo lao Mbeya

Jioni ya jana Disemba 21 Mji wa Mbeya ulizizima kwa shangwe baada ya klabu ya Yanga kutua kuelekea mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc utakaopigwa kesho Jumatano kwenye uwanja wa Sokoine

Ndio! Wakati huu ni raha sana kuwa shabiki wa Yanga kwani jambo moja la uhakika ni kuwa, unapokwenda uwanjani kuwashuhudia vijana wa kocha Cedric Kaze, utarejea nyumbani na furaha

Leo Yanga itafanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Sokoine kuelekea mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali

Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu hivyo kila timu inayokutana nayo, inatamani kuwa timu ya kwanza kushinda dhidi ya vinara hao wa ligi

Ihefu Fc imejiimarisha kipindi hiki cha dirisha dogo ikiongeza wachezaji kadhaa pamoja na ujio wa kocha Zuberi Katwila

Wameshinda mechi mbili zilizopita, mchezo wa mwisho wakiwapiga KMC bao 1-0 hapohapo Sokoine

Hata hivyo itawalazimu wafanye kazi ya ziada kuwadhibiti nyota wa Yanga ambao sasa wamenoga zaidi kutokana ujio wa Saido Ntibazonkiza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’