FT : Ihefu Fc 0-3 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Dec 2020
FT : Ihefu Fc 0-3 Yanga

Yanga imeendelea kugawa vipigo ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Ihefu Fc mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine

Saido Ntibazonkiza ameendea kuwa chachu ya mafanikio kwa Yanga akipika mabao muhimu ambayo yameiweka Yanga mbaali na wapinzani wake katika mbio za ubingwa

Deus Kaseke, Yacouba Sogne na Fei Toto ndio waliyoihakikishia Yanga ushindi muhimu mguu wa Ntibazonkiza ukitengeneza mabao mawili

Ni ushindi ambao unaifanya Yanga ifikishe alama 43, alama 11 zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili

Aidha vijana wa Cedric Kaze wamekamilisha mzunguuko wa kwanza bila ya kupoteza mchezo wowote

Katika michezo 17, wameshinda michezo 13 na kutoka sare michezo minne

Viwanja vya ugenini Yanga imepoteza alama mbili tu!

Wananchi wanarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Singida United

Mchezo huo utapigwa Jumamosi uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’