Ntibazonkiza apewa tuzo Burundi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Dec 2020
Ntibazonkiza apewa tuzo Burundi

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Taifa a Burundi na Umoja wa vijana wa nchi hiyo

Aidha, Ntibazonkiza aliyetua Yanga mwezi uliopita, anatajwa kuwa mchezaji bora kutokea Burundi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita

Ni tuzo anazostahili kabisa kutokana na ubora alioonyesha muda mfupi ndani ya Yanga lakini pia na hata pale anapoitumikia timu ya Taifa ya Burundi

Hapa tunamzungumzia mchezaji ambaye amecheza sio zaidi ya dakika 100 ligi kuu ya Vodacom lakini amehusika katika mabao manne akiwa na kikosi cha Yanga

Pasi tatu za mabao na akaweka kambani bao moja katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji

Huyu ni mchezaji wa kipekee, hakika Burundi ina kila sababu ya kujivunia kuwa mzaliwa wa Taifa hilo

Kwa kuwa na Ntibazonkiza, Yanga imejizolea mashabiki wengi kule Burundi pengine mwishoni mwa msimu itapendeza kama uongozi wa Yanga utaipeleka timu kule Burundi kwenda kuwapa furaha mashabiki wao wapya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’