Klabu ya Polisi Tanzania imepiga hodi pale Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani wakiwahitaji nyota wawili kwa mkopo Waziri Junior na Abdulaziz Makame 'Bui'
Uongozi wa Yanga umeweka bayana kusudio la kuwatoa baadhi ya wachezaji wake kwa mkopo ili wakapate changamoto katika timu ambazo watakuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara
Tayari Juma Mahadhi ameanza kuitumikia Ihefu Fc mchezo wake wa kwanza akicheza dhidi ya waajiri wake Yanga mkoni Mbeya juzi

Makame hayuko katika mipango ya kocha Cedric Kaze wakati Waziri amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Pengine hii itakuwa nafasi kwao kwenda kutumika kwa maafande hao ili waboreshe viwango vyao
ADVERTISE HERE