Yanga imerejea mazoezini jana kuwawinda maafande wa Tanzania Prisons tayari kwa mchezo wa ligi kuu ambao unatarajiwa kufunga mwaka 2020
Mchezo huo utapigwa Disemba 31 uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga
Yanga ilifungua msimu huu wakianza na Prisons, mchezo wa kwanza ukipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa ukimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Wakati huo Yanga ilikuwa ikinolewa na kocha Zlatko Krmpotic. Sasa Wananchi wako chini ya Kocha Cedric Kaze ambaye kwa kiasi kikubwa amekiimarisha kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
Utakuwa mchezo mwenye ushindani, Prisons ni wagumu kufungika huko Sumbawanga. Miongoni mwa michezo waliyoshinda katika uwanja wao ni dhidi ya Simba
Hata hivyo wanakutana na Yanga ambayo haijapoteza mchezo msimu huu. Yanga yenye matokeo mazuri zaidi ugenini
Msimu huu Yanga wamedondosha alama mbili tu ugenini. Kuhakikisha ubingwa unarudi Jangwani, hii ni aina ya michezo ambayo Yanga inapaswa kushinda
Baada ya mchezo dhidi ya Ihefu, uongozi wa Yanga uliamua kuibakisha timu mkoani Mbeya kujiandaa na mchezo huo baada ya mchezo wao wa kombe la FA dhidi ya Singida United kufutwa
Ni Alhamisi ijayo mchezo utapigwa pale uwanja wa Nelson Mandela