Prisons yatamba itavuruga rekodi, Kaze aandaa sapraizi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Dec 2020
Prisons yatamba itavuruga rekodi, Kaze aandaa sapraizi

Licha ya Tanzania Prisons kujinasibu kwamba itatibua rekodi ya Yanga ya kutopoteza mechi hadi sasa, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amesema matokeo ya kumaliza mzunguko wa kwanza kwa kuwa kileleni, yanawapa ari ya kuendeleza ushindi mzunguko wa pili

Yanga ambayo ipo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 43, imemaliza mechi 17 za mzunguko wa kwanza bila kupoteza, ikishinda 13 na kutoka sare michezo minne.

Hata hivyo, juzi Katibu Mkuu wa Prisons, Ajibu Kifukwe, alisema anakumbuka msimu uliopita Prisons ilikuwa ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mechi hata moja kwenye Ligi Kuu, lakini Yanga ndiyo ilitibua rekodi hiyo, kwa hiyo na wao wamejipanga kulipiza kisasi kwa kuwaharibia rekodi yao ya kutopoteza pia.

Lakini Kaze amesema, wachezaji wake watazidi kupambana ili kuwa bora kwenye mechi zao zijazo za mzunguko wa pili.

"Tuna kila sababu ya kushukuru kumaliza mzunguko wa kwanza tukiwa tunaongoza msimamo wa ligi, hii ni kutokana na wachezaji kujitoa na kujitambua kuhakikisha tunapata pointi tatu katika kila mchezo ambazo zimetufikisha hapa.

"Natumaini tutaanza tena vizuri mzunguko wa pili ili tuweze kufanikiwa kufanya vizuri na mwisho wa siku tutwae ubingwa wa ligi,” alisema Kaze.

Timu hizo zitashuka Dimba la Nelson Mandela mjini Sumbawanga keshokutwa, Alhamisi zikiwa na kumbukumbu ya kutoka sara ya bao 1-1 katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’