Kiungo Abdulaziz Makame 'Bui' amepelekwa kwa mkopo kunako klabu ya Polisi Tanzania mpaka mwishoni mwa msimu
Aidha Ruvu Shooting nao wamefanikiwa kumnasa mshambuliaji kinda Adam Kiondo akitarajiwa kuwatumikia kwa miezi sita
Nyota hao wanaungana na Juma Mahadhi ambaye tayari ameanza kung'ara na kikosi cha Ihefu Fc kinachotarajiwa kucheza na Simba baadae leo
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze alipendekeza wachezaji hao watolewe kwa mkopo ili wakapate kuimarisha viwango vyao
Wanaweza kurejeshwa kikosini kama Mrundi huyo ataridhishwa na viwango vyao baada ya msimu kumalizika
ADVERTISE HERE