Muda mchache ujao wananchi watashuka pale uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga kumenyana na Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya kuwa na mwanzo mzuri msimu huu, Yanga imepania kufunga mwaka kibabe kwa kuibuka na ushindi ugenini huko Sumbawanga
Ni mchezo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkali, kwani wenyeji wao Tanzania Prisons nao wamepania kwelikweli
Cedric Kaze kocha mkuu wa Yanga hana presha kuelekea mchezo huo kwani kikosi chake hakikumuangusha katika michezo saba iliyopita
Kaze hatarajiwi kufanya mabadiliko makubwa kwani anaamin katika ile falsafa ya kutobadili timu inayompa matokeo mazuri
Mabadiliko pekee yanayotarajiwa pengine ni kwa wachezaji Saido Ntibazonkiza na Yacouba Sogne ambao walikosa mazoezi kwa siku kadhaa kutokana na majeruhi
Mghana Michael Sarpong anaweza kuanza leo na pengine pia tukamshuhudia Farid Mussa akianza kwenye kikosi cha kwanza
Yanga leo itarajie mchezo wa nguvu kutoka kwa Tanzania Prisons, maafande hawa wa Jeshi la Magereza wanaonekana kukamia sana mchezo huo