Waziri Junior ashauriwa aongeze juhudi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jan 2021
Waziri Junior ashauriwa aongeze juhudi

Msimu uliopita ulikuwa bora sana kwa mshambuliaji Waziri Junior ambaye Yanga ilimsajili akitokea klabu ya Mbao Fc

Pamoja na Mbao Fc kushuka daraja, Waziri aliifungia timu hiyo jumla ya mabao 16 akiwa nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora baada ya kuweka kambani mabao 14 ligi kuu ya Vodacom

Hajawa na mwanzo mzuri kwenye kikosi cha Yanga lakini naamini Waziri bado ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa

Michuano ya kombe la Mapinduzi inaweza kuwa nafasi nzuri kwake kufunga mabao na kujiongezea kujiamini kwani hakuna shaka kocha Cedric Kaze atampa nafasi

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amemsifu Waziri kwa mchezaji mwenye nidhamu kubwa na anayejituma sana mazoezini huku akimtaka afanyie kazi changamoto ndogondogo zinazomkabili ili awe bora zaidi

"Napewa umahiri wako kuanzia upigaji wa vichwa, kufunga kwa ustadi na magoli ya maudhi, umahiri wa kukimbia vizuri kwenye Eneo la Hatari, chenga na hata namna ya kuuficha Mpira"

"Natamani kuona hustuki hata ukikosa nafasi ya wazi ila natamani kuona unayafanyia kazi mapungufu yako na makosa madogo madogo ili uzidi kuimarika na kupata utulivu ila wanayanga wanakuamini mnoo"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’