Ntibazonkiza aongeza mzuka kuelekea mchezo dhidi ya Namungo Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Jan 2021
Ntibazonkiza aongeza mzuka kuelekea mchezo dhidi ya Namungo Fc

Kesho Ijumaa Yanga inakamilisha mechi yake ya pili michuano ya kombe la Mapinduzi wakitarajiwa kuikabili Namungo Fc katika mchezo utakaopigwa saa mbili na robo usiku

Juzi Yanga ililazimishwa suluhu ya bila kufungana na Jamhuri Fc matokeo ambayo yameweka rehani nafasi yao ya kutinga nusu fainali

Yanga inahitaji kushinda mchezo dhidi ya Namungo Fc ili kujihakikishia kucheza nusu fainali. Matokeo ya sare pia yanaweza kuipeleka Yanga nusu fainali kupitia 'best looser' kutegemeana na matokeo ya makundi mengine

Katika mchezo wa kesho, kocha Cedric Kaze anatarajiwa kumtumia kiungo wake mshambuliaji Saido Ntibazonkiza aliyepumzishwa mchezo uliopita

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kwani Namungo Fc wameimarika sana kutokana na ushiriki wao katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Wamerejea jana kutoka Sudan ambako walifanikiwa kutinga raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Al Hilal Obeid kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-3

Lakini pia Yanga na Namungo Fc ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa ligi duru ya kwanza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’