Mara ya mwisho Yanga kufungwa katika mchezo wa ligi kuu ni March 12 2020, dhidi ya KMC wakifungwa bao 1-0
Ni siku 302 zimepita sawa na miezi tisa na siku 27, Wananchi hawajui radha ya kufungwa kwenye ligi
Lakini pia Yanga imecheza siku 180 bila ya kufungwa mchezo wowote sawa na miezi mitano na siku 27
Yanga hawajapoteza mchezo katika michezo 45 waliocheza mfululizo!
Msimu huu tangu walipofungua kwa mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi wakashinda mabao 2-0 dhidi ya Aigle Noir, Yanga hawajapoteza mchezo wowote uwe mashindano au kirafiki
Yani kuna wachezaji kama Kibwana Shomari, Yassin Mustafa, Bakari Nondo, Tomombe Mukoko, Zawadi Mauya, Farid Mussa, Carlinhos, Saido Ntibazonkiza, Yacouba Songne, Michael Sarpong na Tuisila Kisinda, hawa matokeo mabaya waliyopata tangu watue Yanga ni sare tu!
Wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama tisa dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili, Wananchi hesabu zao ni kushinda ubingwa wa 28
Hii ni ahadi iliyotolewa na wadhamini/wahisani GSM, wenyewe wanasema hayupo wa kuwazuia kutimiza lengo hilo