Kimahesabu, Yanga imetinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Namungo Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan
Bao la Zawadi Mauya alilofunga akiwa nje ya 18 kwenye dakika ya 24, lilitosha kuipa Yanga ushindi muhimu ambao unawapeleka nusu fainali
Yanga ilikuwa bora zaidi kwenye kipindi cha kwanza, Kaze akiendelea kutumia mfumo wa 3-4-3


Kipindi cha pili ni Namungo waliokuwa wakishambulia zaidi hata hivyo uimara wa mlinda lango Farouk Shikhalo na safu ya ulinzi iliyokuwa chini ya Said Juma Makapu, waliweza kuondoa hatari zote langoni
Yanga ilihitaji kushinda mchezo huu ili kusonga mbele, matokeo haya yamewahakikishia kusonga mbele
ADVERTISE HERE