Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga Injinia Hersi Said amesema kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa, kutakuwa na utambulisho wa wachezaji wapya
Aidha Hersi amedokeza kuwa wako katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mchezaji mmoja wa ndani, wakati wowote atatambulishwa
Bila ya kutaja klabu anayotokea, Injinia Hersi amewataka mashabiki wakae tayari kumpokea
"Nawapa taarifa rasmi kuwa tuko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mchezaji mmoja ambaye muda si mrefu atakaa kwenye lile kochi jeupe. Siwezi kusema anatokea klabu gani lakini ni ndani ya nchi," Hersi aliwaambia Wanahabari baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc jana
Tangu dirisha dogo la usajili lilipofunguliwa, Yanga imehusishwa na wachezaji kadhaa ambapo mashabiki wanamsubiri Injinia Hersi kufanya utambulisho wa nyota hao
Β