Mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi utawakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba, keshokutwa Jumatano Januari 13 2020
Simba imeifuata Yanga fainali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa pili wa nusu fainali
Yanga ilitangulia fainali mapema kwa kuigaragaza Azam Fc kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1
Mashabiki wa Yanga walikuwa na shauku kubwa kuwaona watani zao wakishinda ili waweze kukutana nao fainali
Sasa miamba hao wa soka wanakumbana Jumatano katika mchezo utakaopigwa kuanzia saa mbili na robo usiku
ADVERTISE HERE