Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati inayohusika na usajili Yanga, amesema watakamilisha usajili wa mshambuliaji wa kigeni
Jana Yanga ilitambulisha usajili wa beki kiraka Dickson Job kutoka Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili na nusu
Hersi amesema Wananchi wajiandae kwenda JNIA kumpokea mshambuliaji mwingine
"Jana tumetambulisha mchezaji mmoja lakini bado hatujamaliza usajili. Kabla ya dirisha dogo kufungwa utambulisho mwingine utafanyika. Ni mchezaji wa kigeni, Wananchi wajiandae kwenda 'Airport'," alitamba Hersi
Dirisha dogo la usajili litafungwa Ijumaa saa 5:59 usiku, siku tatu zikiwa zimesalia
Β
Β
ADVERTISE HERE