Watani wa jadi Simba na Yanga wanakutana leo kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi
Ni mashabiki 12,000 tu ambao wataruhusiwa kuingia uwanja wa Amaan kushuhudia mchezo huo hali iliyopelekea kupanda kwa viingilio vya mchezo huo
Tangu kuanza kwa michuano ya mwaka huu, tiketi ziliuzwa kwa Sh 3000, 5000 na 10,000 lakini leo zinauzwa kuanzia Sh 5000, 10000 na 15000
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mchezo huo utakaounguruma kuanzia saa mbili na robo usiku
ADVERTISE HERE