Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Yanga kushinda ubingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya watani zao Simba baada ya mchezo wa fainali kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Kocha Cedric Kaze alifanikiwa kimbinu kwani Yanga iliukamata mchezo wakitengeneza nafasi tano za kufunga ukilinganisha na watani zao Simba ambao hawakupiga hata shuti moja lililolenga lango



Ni matokeo ambayo Yanga walistahili kutokana na jitihada zilizoonyeshwa na wachezaji uwanjani
Walinzi Said Juma Makapu na Abdallah Shaibu 'Ninja' wanaweza kuwa wamempa mtihani kocha Kaze kutokana na kiwango bora walichoonyesha kwenye mchezo huo
Mikwaju ya penati ya Yanga iliwekwa kambani na Zawadi Mauya, Ninja, Tuisila Kisinda na Saido Ntibazonkiza wakati Mukoko Tomombe alikosa
Meddie Kagere na Joash Onyango walikosa mikwaju yao kwa upande wa Simba, kwa mara nyingine Farouk Shikhalo akiibuka shujaa
Shikhalo ameshinda tuzo ya golikipa bora wa mashindano