Jana Yanga imeanza kuhesabu mataji mwaka huu 2021 baada ya kushinda kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 baada ya mchezo kumalizika dakika 90 kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Kiungo mkabaji Mukoko Tomombe ni miongoni mwa wachezaji waliojitoa kwelikweli kwenye mchezo huo kuhakikisha ushindi unapatikana
Pamoja na Mama yake kuwa mgonjwa sana, Mukoko alibaki visiwani Zanzibar kushiriki Mapinduzi Cup na muhimu zaidi akawa sehemu ya kikosi kilichopata ushindi dhidi ya Simba
Hakuwa na bahati kwenye mikwaju ya penati lakini juhudi zake zilionekana ndani ya dakika 90
Hata baada ya Yanga kushinda, wachezaji wenzake walilazimika kumtuliza kutokana na hisia kali zilizomtawala
Mukoko ni mchezaji wa mfano katika kikosi cha Yanga, jana ameonyesha kwa kiasi gani anaiheshimu, kuithamini na kuipenda klabu ya Yanga
Injinia Hersi Said atakuwa na furaha kubwa kwa usajili wa nyota huyu, kwani Mukoko amekuwa Mwananchi hasahasa, anaipigania timu na kuongoza wenzake akiwa ndani ya uwanja
Tunamuombea kheri Mama Mukoko aweze kupona maradhi yanayomsumbua na muhimu tunamshukuru kwa kutuletea jembe hili duniani