Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka mashabiki wake wa jijini Dar es salaam kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya timu yao saa saba Bandarini
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema mabingwa hao wa michuano ya kombe la Mapinduzi wataondoka visiwani Zanzibar leo na kuwasili Dar saa saba na nusu mchana
"Timu itawasili mchana wa leo. Wanachama na mashabiki wetu wafike kwa wingi Bandarini kwa ajili ya mapokezi ya kikosi na kombe la Mapinduzi tuliloshinda juzi."
"Baada ya kuwasili msafara utaelekea moja kwa moja Makao Makuu ya klabu ambako viongozi watazungumza mambo kadhaa na Wanachama na mashabiki wetu"
"Tutawataarifu barabara ambazo msafara wetu utakuwa umeruhusiwa kupita lakini inaweza kuwa hii ya Mnazi Mmoja mpaka Kariakoo au ile inayozungukia faya," alifafanua Bumbuli
Katika hatua nyingine Bumbuli amesema mashabiki wakae tayari kumpokea mshambuliaji mpya wa kigeni kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa usiku wa leo
Bumbuli amesema pamoja na kuwa na tukio kubwa la kuipokea timu inayowasili kutoka visiwani Zanzibar, lakini Wananchi wasiwe na hofu kwani wakati wowote watataarifiwa usajili wa mchezaji huyo
"Leo hatutaki kuchanganya shughuli mbili lakini niwaambie wanachama na mashabiki wetu, kuna jambo kubwa litatokea kabla ya dirisha la usajili kufungwa, wakae tayari.."