Mfahamu Fiston Abdul Razak jembe jipya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jan 2021
Mfahamu Fiston Abdul Razak jembe jipya Yanga

Jana Yanga ilifunga dirisha dogo kwa kumsajili mshambuliaji Kimataifa wa Burundi Fiston Abdul Razak akitua kwa Wananchi akitokea klabu ya ENPPI inayoshiriki ligi kuu ya Misri

Fiston ametua Yanga akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na ENPPI

Huyu ni pacha wa Saido Ntibazonkiza kwenye timu ya Taifa ya Burundi

Pamoja na kufanya vizuri sana msimu huu, kikosi cha Yanga kimekabiliwa na changamoto katika safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Mghana Michael Sarpong akishirikiana na Yacouba Songne na Waziri Junior

Lilikuwa hitaji la kocha Cedric Kaze kupata mshambuliaji mwingine ambaye ataiongezea safu yake makali

Ujio wa Fiston ni pendekezo la Kaze mwenyewe, bila shaka eneo hilo la ushambuliaji linakwenda kupata tiba

Fiston ana uwezo wa kucheza nafasi zote za winga, ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika

Akiwa na umri wa miaka 27, Fiston ameshiriki ligi zenye ushindani katika nchi za Afrika Kusini na Misri

Msimu wa 2015/16 Fiston alisajiliwa na klabu ya Mamelodi Sundowns akitokea Sofapaka ya Kenya. Aliitumikia timu hiyo kwa misimu miwili ikiwa ni pamoja na kutolewa kwa mkopo katika klabu ya Celtic ya huko huko Afrika Kusini

Katika misimu miwili aliyokuwa Afrika Kusini, Fiston alifunga mabao 15 katika mashindano yote

Mwaka 2017 akasajiliwa na mabingwa wa Angola 1 De Agosto ambao aliwatumikia kwa msimu mmoja kabla ya kutimkia Al Zawraa ya Iraq

Alipotoka Iraq akaitumikia JS Kabylie ya Libya kwa muda mfupi kabla ya kujiunga na ENPPI ya nchini Misri aliyoitumikia mpaka Novemba 01, 2020 mkataba wake ulipomalizika

Akiwa na timu ya Taifa ya Burundi, Fiston amecheza mechi 33 akiweka kambani mabao 16

Huyu ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa, hakuna shaka ujio wake Yanga utakuwa na faida kubwa hasa katika eneo la ushambuliaji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’