Fiston atamba atan'gara Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jan 2021
Fiston atamba atan'gara Tanzania

Mshambuliaji mpya wa Yanga Fiston Abdul Razak amesema atapambana kuhakikisha anafanya vizuri ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria katika ligi kuu ya Vodacom

Fiston alisajiliwa na Yanga juzi muda mfupi kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba kule Misri klabu ya ENPPI

Nyota huyo alisaini mkataba wa miezi sita ambapo kuna makubaliano ataongeza mwishoni mwa msimu kama mabosi wataridhishwa na uwezo wake

Moja ya changamoto inayowakabili nyota wengi wa kigeni wanaokuja kucheza Tanzania ni kushindwa kufanya vizuri katika ligi kuu ya Vodacom licha ya kufanya vizuri huko walikotoka

Fiston raia wa Burundi amesema kwa upande wake amejiandaa vizuri na ana hakika atawapa furaha mashabiki

"Zipo sababu ambazo zinaweza kupelekea mchezaji asifanye vizuri anapohama kutoka ligi moja kwenda nyingine. Kwanza ni maandalizi kwa mchezaji mwenyewe. Ni muhimu kwa mchezaji mwenyewe kujiandaa na kuwa tayari kwa ajili ya changamoto mpya"

"Lakini pia ni vile mchezaji mwenyewe alivyo. Wachezaji tuna tofautiana, kuna wengine wanazoea mazingira mapya kwa haraka lakini wengine wanahitaji muda kuzoea kabla ya kuanza kufanya vizuri"

"Pia suala la ushindani wa ligi linachangia. Kwa upande wangu naifahamu ligi ya Tanzania, nimejiandaa vizuri, nitahakikisha nawapa furaha mashabiki," alisema Fiston

Pamoja na kucheza nafasi ya ushambuliaji, Fiston maarufu 4G pia humudu kucheza nafasi zote za winga

Unaambiwa mwamba huyu ana kasi mithiri ya Tuisila Kisinda ndio maana wakampachika jina la 4G

Sisi vuta taswira, kwa Kisinda tu mabeki wanateseka vile itakuwaje akiongezeka na Fiston

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’