Yanga haina presha ya usajili

Admin By Admin
β€’
12 Dec 2017
Yanga haina presha ya usajili
Wakati dirisha dogo la usajili likielekea ukingoni, kumekuwa na hofu miongoni mwa mashabiki wa Yanga wakiamini mabingwa hao watetezi ligi kuu ya Vodacom walipaswa kuwa 'busy' sana sokoni kusajili wachezaji wapya.

Lakini ifahamike kuwa kwa ujumla kikosi cha Yanga kilikuwa na mapungufu machache sana ambayo kimsingi yamefanyiwa kazi.

Hofu pekee iliyoko ni kwa wachezaji majeruhi ambao nao imeelezwa upo uhakika watarejea dimbani mapema.

Mpaka sasa zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa Yanga imesajili wachezaji wawili tu,beki wa kati raia wa DRC Fiston Kayembe Kanku na mshambuliaji Yohana Mkomola aliyesajiliwa akitokea Academy ya Etoile Du Sahel.

Mshambuliaji Donald Ngoma ni kama amemalizana na uongozi wa Yanga kwani tayari ameruhusiwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza.

Amissi Tambwe hali yake imeimarika zaidi na huenda akawa tayari kuanza kuitumikia Yanga katika mchezo dhidi ya Mbao FC, Disemba 29.

Hofu pekee iko sehemu ya kiungo ambayo matumaini ni kwamba Thabani Kamusoko atapona majeraha yake mapema na kuweza kurejea dimbani.

Ili kuweza kusajili mchezaji wa Kimataifa Yanga italazimika kuvunja mkataba wa mmoja wa wachezaji wake wa Kimataifa na bila shaka italazimika kulipa fedha nyingi.

Ikumbukwe ukimuondoa Obrey Chirwa, wachezaji wengine wote wa Kimataifa walisaini mikataba ya miaka miwili kuitumikia Yanga kuanzia mwezi Julai, 2017.

Hii ni changamoto kwa uongozi hasa ukizingatia hali ya kiuchumi ya klabu kwa hivi sasa.

Kocha George Lwandamina amedhihirisha anaweza kutengeneza kikosi imara bila ya kutegemea wachezaji wenye majina.

Bila shaka Lwandamina ameridhika na kikosi alichonacho.

Na ndio maana amezuia baadhi ya wachezaji waliokuwa wanatakiwa kwa mkopo na vilabu vingine.

Yanga ni miongoni mwa timu zinazoundwa na wachezaji vijana zaidi katika ligi kuu ya Vodacom.

Ukiondoa wakongwe kama Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Thabani Kamusoko na Amissi Tambwe kikosi cha Yanga kimesheheni wachezaji vijana wenye uchu wa mafanikio.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
27m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’