Tumeongeza majembe ya kazi - Mwambusi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jan 2021
Tumeongeza majembe ya kazi - Mwambusi

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema usajili ambao umefanywa katika safu yao ya ushambuliaji, sasa unawapa jeuri ya kutamka kwamba, hakuna timu itakayowazuia kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara

Mwambusi aliyewahi kutamba akiwa kocha wa Mbeya City, amesema msimu huu wako vizuri na wana imani kwa mwenendo wa timu yao hakuna itakayowasumbua.

Alisema malengo yao makubwa msimu huu ni kufanya vizuri kila mechi iliyopo mbele yao na kwamba baada ya kutwaa Kombe la Mapinduzi sasa wako imara zaidi kwa ajili ya Ligi Kuu.

"Tumefanya usajili wa wachezaji watatu, Saidi Ntibazonkiza ambaye tayari ameonekana makali yake, lakini pia kuna Dickson Job na tumefunga dirisha kwa kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa Fiston Abdul Razak.

"Tumeongeza watu wa kazi watakaoleta ushindani na kuimarisha kikosi, ninaimani tutakaporejea kutoka mapumziko tunaendelea tulipoishia ni kutafuta pointi tatu kila mechi," alisema Mwambusi

Baada ya kurejea kutoka visiwani Zanzibar kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaza aliwapa wachezaji mapumziko ya siku 10, wote watarejea kambini wiki ijayo kuendelea na maandalizi ya mzunguko wa pili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
26m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’