Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli ameitwa Kamati ya Maadili kujieleza kwa kile kilichoelezwa kuwa amekaidi adhabu ya kulipa faini ya Tsh Milioni tano aliyopewa na TFF wakati wa sakata la usajili wa Bernard Morrison
Katika sakati hilo ambalo lilimalizika kwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kubatilisha mkataba wa Morrison na Yanga, Bumbuli aliadhibiwa kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo wakati shauri hilo likiendelea
Kwa mujibu wa Kakuni za Maadili za TFF toleo la Mwaka 2013, baada ya kutoridhika na adhabu hiyo, Bumbuli aliomba sababu za maamuzi (Grounds of decision) na Mwenendo wa mashtaka (proceedings) ili aweze kukata rufaa, toka mwezi wa kumi mwaka jana mpaka sasa hakuna alichopatiwa
Kanuni ya 70 (1) ya kanuni tajwa zinampa haki Bumbuli kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Maadili kwenda kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili, hivyo Kamati ya Maadili hupoteza mamlaka juu ya suala husika
Sasa wakati hilo likiwa halijafanyika, TFF wanamuita tena kwenye kamati ya Maadili licha ya kuwa amefuata taratibu zote za kisheria kupata haki yake ya kukata rufaa