Mchakato wa mabadiliko Yanga kuanza leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
13 Dec 2017
Mchakato wa mabadiliko Yanga kuanza leo
Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga inatarajiwa kukutana leo Jumatano, Disemba 13 kuandaa maandalizi ya kuanza mchakato wa kufanya mabadiliko katika klabu hiyo.

Hivi karibuni baada ya klabu ya Simba kukamilisha mchakato wa kufanya mabadiliko ya kiuendeshaji, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga alisema Yanga iliuanza mchakato huo muda mrefu.

Akihojiwa na redio moja ya jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Sanga alisema kimsingi mabadiliko ya uendeshaji wa klabu za soka nchini ni muhimu katika maendeleo ya soka.

“Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 13, mwaka huu kuanza mchakato wa kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu yetu, tutalifikisha hili kwa wanachama,” alisema Sanga.

Sanga alisema mchakato huo katika klabu yao ulianza muda mrefu, lakini ulisimama kwa sababu mbalimbali.

“Katiba yetu ambayo tuliifanyia marekebisho mwaka 2010, inaruhusu mabadiliko haya, lakini hapo awali kulikuwa na suala la kampuni ndani ya klabu kwa maana ya kuwa na klabu kama klabu na pia kuwa na kampuni... hivyo jambo kama hili litazungumzwa kwa wanachama kuona nini tunaamua,” alisema Sanga.

Alisema wataamua kama klabu ijiendeshe kama kampuni au kuwapo kwa kampuni ndani ya klabu ya Yanga ambayo inadhaminiwa na SportPesa.

Alisema wazo la kuwa na kampuni lilikuwapo Yanga kwa miaka ya nyuma, lakini halikuendelezwa kwa sababu mbalimbali.

Sanga, alisema baada ya mkutano huo wa kamati ya Utendaji utaitishwa mkutano wa wanachama kwa ajili ya kuwasilisha hoja hiyo.

Kama Yanga itaanzisha mchakato huo na kufanikiwa kuukamilisha, watakuwa wamekamilisha hatua ambayo Simba wameifikia ya kubadili uendeshaji wa klabu yao kutoka kuwa Simba SC na kuwa Simba SC Limited kwa kuuza hisa za klabu hiyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →