Kamati Mashindano ya Kombe la Mapinduzi imetangaza Mapato yaliyopatikana katika Mchezo wa Fainali ya Kombe hilo kati ya Simba na Yanga uliochezwa January 13, 2021 katika Uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar
Fedha zilizopatikana katika mchezo huo ni Shilingi Milioni 79, laki 2 na elfu 45
Aidha, kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Kamati hiyo Bibi Imane Duwe amesema Jumla ya Shilingi Milioni 496, laki 1, elfu 78 na mia 4 wamekusanya katika Mashindano kutoka kwa Wadhamini na Viingilio vya Milangoni ambapo baada ya kulipa matumizi yote wanatarajia kubakisha Shilingi Milioni 141, laki 7 na elfu 3 ambazo watazirejesha Serikalini
Yanga waliibuka mabingwa wa michuano hiyo wakiwafunga watani zao Simba kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana