Beki mpya wa Yanga Dickson Job kwa mara ya kwanza jana alishiriki mazoezi ya kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria yaliyoanza kule Kigamboni
Job aliyesajiliwa na Yanga usajili wa dirisha dogo akitokea Mtibwa Sugar, alieleza furaha yake baada ya kujiunga na Yanga
"Nimefurahi leo nimeanza mazoezi na timu yangu ya Yanga. Ilikuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu kupata nafasi ya kucheza timu kubwa kama Yanga. Nashukuru tumefanya mazoezi vizuri, nimepata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi na wachezaji wenzangu naamini kwa umoja huu tutafanya vizuri katika mzunguuko wa pili"
"Kwangu mimi mashabiki watarajie makubwa kwani Watanzania wameniamini na sasa napaswa kuthibitisha kile nilichikuwa nikifanya Mtibwa Sugar.
"Nawaambia mashabiki wa Yanga watafurahi kwani nimejipanga kufanya vizuri katika timu hii kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu ili tuweze kuchukua ubingwa msimu huu," alisema Job


Job alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha timu ya Taifa lakini hakusafiri na timu kule Cameroon baada ya kupata majeraha
Hata hivyo nahodha huyo wa timu ya Taifa ya vijana (U-20) amepona majeraha na sasa ameanza majukumu yake ndani ya kikosi cha Yanga