Yanga kukata rufaa adhabu ya Bumbuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jan 2021
Yanga kukata rufaa adhabu ya Bumbuli

Uongozi wa klabu ya Yanga unakusudia rufaa kupinga kufungiwa kwa Afisa wake wa Habari Hassan Bumbuli

Jana Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilitangaza kumfungia Bumbuli kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitatu ndani na nje ya nchi kwa kile walichoeleza kukaidi adhabu ya kulipa faini ya Tsh Milioni Tano aliyopewa na Kamati ya Maadili

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya kufungiwa, Bumbuli amesema klabu haijaridhishwa na adhabu hiyo na watatumia haki yao ya kukata rufaa

"Adhabu nimeiona, tumeipokea. Kama uongozi kwanza hatujaridhika, hiyo ni hatua ya kwanza, hatua ya pili itafuata kwa sababu kuna nafasi ya kukata rufaa na tutakata rufaa," alisema

Aidha Bumbuli amethibitisha kuwa tayari alishalipa faini ya Tsh Milioni Tano, na stakabadhi ya malipo aliiwasilisha TFF

"Nililipa faini na pay slip nilipeleka TFF ikapokelewa na Mhasibu, kwa bahati mbaya akasema hakuwa na risiti kwa muda ule kwa hiyo risiti nitaifata. Sisi copy za pay slip tunazo"

"Viongozi wa TFF walikuwa na taarifa kuanzia wanasheria wa TFF, tukaenda kwenye Kamati nikawaambia kila kitu kwa hiyo kila mmoja alikuwa anataarifa hiyo pesa imeshalipwa," alisema

"Hilo suala la kukaidi halikuwepo, tulikuwa tumedhamiria kukata rufaa lakini kwa bahati mbaya hatukupewa vitu tulivyokuwa tunavihitaji kwa ajili ya kukata rufaa kwa wakati ambao tulikuwa tunahitaji"

"Lakini pia hata hukumu haikuonesha chochote kwamba natakiwa kulipa faini ndani ya muda gani, barua ilieleza kwamba natakiwa kulipa faini, sitakiwi kufanya kosa la kimaadili ndani ya miaka miwili na nina haki ya kukata rufaa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’