Kiungo fundi Carlos Stenio Fernandes Guimaraes do Carmo 'Carlinhos' amerejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki 12
Carlinhos ameshiriki mazoezi yote Yanga yaliyoanza Jumatatu Januari 25 baada ya mapumziko ya siku 10
Mwamba huyu amerejea akiwa na ari akifahamu ana deni kubwa kwa mashabiki wa klabu ya Yanga
Usajili wake ulitikisa nchi, lakini Wananchi bado hawajapata kile walichokitarajia sababu ya majeraha yaliyomfanya acheze mechi chache sana
Kurejea kwake kumeongeza ushindani katika eneo la kiungo cha ushambuliaji eneo ambalo pia wapo Saido Ntibazonkiza, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke


Katika mechi sita alizocheza kwenye ligi, Carlinhos amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao
ADVERTISE HERE