Benchi la ufundi la Yanga limesheheni makocha vijana lakini pia makocha hawa wanazo elimu zilizowafanya waajiriwe na mabingwa hao wa kihistoria
Kocha wa viungo Edem Mortotsi ni miongoni mwa makocha hao wa Yanga ambao baaado damu 'inachemka'
Akiwa na umri wa miaka 27 tu, Mortotsi amefuzu mafunzo ya ukocha pia akiwa na diploma ya masuala ya usimamizi wa mazoezi ya utimamu mwa mwili
Mwenyewe amefichua kuwa aliipenda kazi hiyo tangu alipokuwa mdogo na alianza mafunzo mapema na mwaka uliopita alipata cheti chake cha Diploma
Kocha huyo ambaye anaongoza kitengo cha 'fitnes' ya wachezaji, amesema amekuja nchini kufanya kazi moja tu, kuhakikisha anawaweka wachezaji sawa muda wote kwa ushindani
"Hakuna kitu ninachofikiria zaidi ya kushinda, Hivyo nitafanya kazi wakati wote kuhakikisha tunashinda kila kitu," alisema Mortotsi