Mshambuliaji mpya wa Yanga Fiston Abdul Razak ambaye alisajiliwa katika usajili wa dirisha dogo, amekabidhiwa jezi namba saba iliyokuwa ikitumiwa na kiungo mshambuliaji Mapinduzi Balama ambaye ni majeruhi
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela ametoa ufafunuzi kuwa sio tatizo kwa Fiston kutumia jezi hiyo na kuwa Balama atakaporejea anaweza kupewa jezi nyingine
"Sioni tatizo kwa Fiston kutumia jezi namba saba, hili ni suala la kawaida kabisa. Balama atakaporejea atakabidhiwa jezi nyingine. Wapo watu wanajaribu kulikuza hili ionekane Balama hatendewi haki lakini niwaambie, Yanga tunamthamini mchezaji wetu na naamini atarejea dimbani karibuni"
"Baada ya kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini, sasa anauguza kidonda tu na atakapopona atarejea uwanjani. Atakabidhiwa jezi nyingine, hakuna tatizo"
Mwakalebela amesema Balama atarejea uwanjani kabla ya msimu huu kumalizika