Mashabiki wa Yanga kesho Jumamosi watakuwa na nafasi ya kumshuhudia 'mbashara' mshambuliaji wao mpya Abdul Razak Fiston katika mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports kutoka jijini Tanga
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Azam Complex kuanzia saa moja usiku
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewaalika mashabiki kujitokeza kwa wingi kushudia mtanange huo wa kwanza baada ya mapumziko ya CHAN
Ni viingilio vya Tsh 5,000/- VIP na Tsh 3,000/- mzunguuko
Huu ni mchezo wa kujipima nguvu, kocha Cedric Kaze akijaribu mbinu zake kabla ya kurejea kwa mikiki mikiki ya ligi kuu wiki ijayo
ADVERTISE HERE