Licha ya kasi yake ya kufunga mabao kusuasua, Mshambuliaji wa Yanga Michael Sarpong amesema hana presha sana kwani anaamini ni suala la muda tu
Lakini muhimu zaidi kwake ni kuona timu inafanya vizuri akiahidi kuendelea kupambana katika michezo iliyobaki
"Nafikiri kiwango cha ufungaji hakipo chini kwa mtazamo wangu, kwani bado najaribu na nina matumaini, nafikiri raundi hii kutakuwa na tofauti"
"Kuhusu presha katika hilo la ufungaji kwangu mimi sina presha, sidhani kama ni tatizo kwa sababu timu inaposhinda ni vizuri zaidi kwani klabu ni kubwa kuliko mchezaji yeyote," alisema
Sarpong ameweka kambani mabao manne kwenye ligi akiwa amefunga jumla ya mabao sita katika mechi zote alizocheza tangu aliposajiliwa na Yanga
ADVERTISE HERE