Kaze ataka utulivu mechi ya Kagera Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Feb 2021
Kaze ataka utulivu mechi ya Kagera Sugar

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, amewataka wachezaji wake kusahau matokeo ya mechi iliyopita na badala yake kuwekeza akili na nguvu katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam

Timu zote mbili zitashuka dimbani kesho zikiwa na kumbukumbu ya kugawana pointi, tena wapinzani wao wakisawazisha dakika za lala salama, Kagera Sugar ikibanwa na Gwambina FC huku Mbeya City ya jijini Mbeya ikiwa nyumbani iliwasimamisha vinara hao.

Kaze amesema amewaelekeza wachezaji wake kuondoa mawazo kuhusiana na mechi iliyopita na sasa wanatakiwa kupambana kuvuna pointi tatu za mchezo uliopo mbele yao.

Kocha huyo raia wa Burundi amesema mechi zote za mzunguuko wa pili hazitakuwa rahisi hivyo wachezaji wanatakiwa kuongeza umakini na kujitoa katika kila dakika ya mchezo ili kufikia malengo.

"Tumerejea nyumbani na kufanya mazoezi mara mbili (asubuhi na jioni), kwa ajili ya kujiweka sawa, ligi ni ngumu na tunahitaji kupambana kuhakikisha tunafikia malengo yetu, kazi iliyoko mbele ni kubwa, hatutakiwi kukata tamaa," alisema Kaze.

Kaze amesema kila mchezaji anajua majukumu yake akiwa ndani ya uwanja na anawaamini vijana wake watakamilisha mikakati waliyonayo ili kuona wanapata ushindi na hatimaye kuibuka mabingwa wa msimu huu wa 2020/21.

"Tunatakiwa kupambana na vile vile kuwa makini, kuongeza utulivu kwa kutumia nafasi tunazozitengeneza, hakuna mechi rahisi kwa sasa kila timu inahitaji kupata pointi, tunaangalia maandalizi yetu pamoja na nguvu kubwa kwenye kusaka ushindi ndani ya dakika 90," alisema Kaze

Kuhusiana na Saidi Ntibanzokiza, amesema hatakuwa sehemu ya mpango wa mechi hiyo kwa sababu anaendelea na matibabu huku golikipa, Ramadhani Kabwili na mlinzi, Abdallah Shaibu 'Ninja' wakirejea kikosini baada ya afya zao kuimarika.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’