Msemaji na Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza mapema uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Jumatano kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Nugaz amesema kuanzia saa 11 jioni kutakuwa na tukio maalum ambalo litafanyika kabla ya kuanza kwa mchezo wa Kagera Sugar saa moja usiku
"Kesho Uwanja wa Mkapa hapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni tuna jambo letu kabla ya Mchezo wetu dhidi Kagera Sugar wanachama,wapenzi na Mashabiki wa Yanga tujitokeze kwa wingi sana," amesema Nugaz
Ni tukio la hafla fupi ya kusherehekea miaka 86 ya klabu ya Yanga toka kuanzishwa kwake itakayofanyika ndani ya uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE