Mtihani mwingine kwa Fiston leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Feb 2021
Mtihani mwingine kwa Fiston leo

Mshambuliaji mpya wa Yanga Fiston Abdul Razak leo atakuwa na nafasi nyingine ya kuonyesha ubora wake wakati Wananchi watakaposhuka dimbani kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Fiston ameitumikia Yanga katika michezo miwili , mmoja ukiwa na kirafiki dhidi ya African Sports na mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City

Bado nyota huyo wa timu ya Taifa ya Burundi hajaonyesha makali yake lakini mashabiki wameweka matumaini makubwa kwake kwani ujio wake ulilenga kuboresha safu ya ushambuliaji

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema hana wasiwasi na uwezo wa Fiston, ni suala la muda tu ataanza kuonyesha kile kilichopelekea wamsajili 

Fiston mwenyewe anaamini kwa ubora wa wachezaji wanaounda kikosi cha Yanga akishirikiana nao vema wanaweza kupata matokeo chanya kwa kufunga mabao wanapopata nafasi

"Kwa ujumla ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata matokeo chanya ndani ya uwanja, bado tuna muda wa kufanya vizuri na mashabiki watafurahi," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’