Mkomola kuanza mchezo wa Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Dec 2017
Mkomola kuanza mchezo wa Jumapili
Mshambuliaji mpya wa Yanga Yohana Mkomola anatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Jeshi la Polisi la Tanzania keshokutwa Jumapili.

Mshambuliaji huyo kinda alijiunga na kikosi cha Yanga katikati ya wiki hii baada ya kurejea kutoka Kenya alikokuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars'.

Licha ya umri wake mdogo, Mkomola ametabiriwa kuja kuwa mmoja wa washambuliaji tishio katika ligi kuu ya Vodacom.

Wengi wamekuwa wakimfananisha na nahodha wa timu ya Taifa, Mbwana Samatta ambaye sasa anakipiga na KRC Genk inayoshiriki ligi kuu ya Ubelgiji.

Hata Samatta mwenyewe aliwahi kumtabiria mafanikio makubwa Mkomola ambaye alikutana nae kwenye kikosi cha timu ya Taifa.

Hivi karibuni kocha wa Lipuli FC Selemani Matola alisifu usajili wa kinda huyo uliofanywa na Yanga kwa kusema ndio usajili bora uliofanywa na timu katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Mkomola alin'gara katika michuano ya AFCON chini ya umri wa miaka 17, michuano iliyofanyika nchini Gabon mapema mwaka huu.

Ndani ya kikosi cha Yanga Mkomola amekaidhiwa jezi namba 31.

Mchezaji mwingine mpya ambaye anatarajiwa kucheza mchezo huo ni mlinzi wa kati Fiston Kayembe.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’